Biashara na Uchumi : Ridhiwani Kikwete Atoa wito kwa Makampuni ya Mawasiliano Kusambaza Huduma kwa Wateja wake - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Dec 2014

Biashara na Uchumi : Ridhiwani Kikwete Atoa wito kwa Makampuni ya Mawasiliano Kusambaza Huduma kwa Wateja wake


Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,(kulia)Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wapili kutoka kulia ,akigonganisha glasi za mvinyo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania ikiwa ni ishara ya kusherehekea uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo alilolizindua lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto)akimfafanulia jambo Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofika kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kulia kwa Mheshimiwa ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa wa Pwani.
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wanne toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Chalinze mjini Mkoani humo. 
 
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani  Mh. Ridhiwani Kikwete,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano  kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo  Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya Ruvu,Miono,Gwata  wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imefungua duka jipya  katika  eneo la Chalinze.

Chalinze  ni moja ya kituo maarufu katika  mkoa wa Pwani ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Chalinze na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa  mballimbali na nje ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard   wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka  85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa pwani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad