Uchumi Wetu : Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ya TRA lafanyika ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Nov 2014

Uchumi Wetu : Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ya TRA lafanyika ,Jijini Dar


Kaimu Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.Picha zote na Othman Michuzi.

Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika Novemba 15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.



Sehemu ya Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akifatilia kwa makini michezo mbali mbali iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo.
MC wa Bonanza akiendelea na Wajibu wake.
Team nzima ya Michuzi Media Group katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad