Matukio ya Moto Arusha: Taswira ya Moto ulivyoteketeza Soko la Vinyago (Mt. Meru Curios & Craft Market ) ,Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Nov 2014

Matukio ya Moto Arusha: Taswira ya Moto ulivyoteketeza Soko la Vinyago (Mt. Meru Curios & Craft Market ) ,Jijini Arusha


Makamu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.



Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.



"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao wako mita chache na  yalipo maduka haya"amesema Mulongo



Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog



Watu wakiokoa baadhi ya mabaki ya Bidhaa hizo
Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET ,Jijini Arusha.

Vijana wakionekana wakiokota baadhi ya bidhaa zilizosalia


Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad