Maoni Binafsi : Blogger wa Kimataifa Jeff Msangi aandika Yake kuhusu Rasimu ya Katiba - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Nov 2014

Maoni Binafsi : Blogger wa Kimataifa Jeff Msangi aandika Yake kuhusu Rasimu ya Katiba

Jeff Msangi ; kutoka Facebook Page: Kama nia ni kuhahakikisha kwamba wananchi wanaendelea kuwa "vipofu", basi muhimu ni kukumbushana kwamba katika zama za leo,haiwezekani. Nimenukuu hiki kipande mahali...

"Awali, Jaji Warioba, alisema asilimia 81 ya ibara za Rasimu ya Tume yamo kwenye katiba inayopendekezwa, hata hivyo, maudhui yake yakitazamwa kwa makini mambo mengi ya msingi yametupwa.

Aliyataja mambo manne ya msingi yenye kuleta mabadiliko ambayo yalipendekezwa na wananchi yaliyoondolewa kuwa ni tunu za maadili ambazo kwa mujibu wake, zilibadilishwa na kuwa urithi, madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka kutengenisha mihimili ya Serikali na Bunge na Muundo wa Muungano.

Alisema kuna baadhi ya mambo yaliyopo kwenye katiba inayopendekezwa yanatia shaka iwapo yatakuwa katika utekelezaji yakiwamo mgombea binafsi na asilimia 50 kwa 50 ya wabunge wanawake na wanaume.
Kuhusu kura ya maoni alisema ni lazima wananchi waandikishwe kwanza kwenye daftari la kupiga kura huku akiwataka kuwa makini kuyapigia kura mambo ya msingi."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad