Kutoka Bungeni :Mhe. Zitto Kabwe Awasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Bungeni Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Nov 2014

Kutoka Bungeni :Mhe. Zitto Kabwe Awasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Bungeni Dodoma

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu akauti ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akienda kusoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma.

Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya Mkaguzi wa hesabu za serikali Bungeni.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya hiyo kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti hiyo kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Deo Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka tarehe 27 Novemba 2014 ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad