Elimu na Maisha : Doris Mollel Achangia Vitabu kwa Ushirikiano na MAK Solutions ,Mpunguzi Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Nov 2014

Elimu na Maisha : Doris Mollel Achangia Vitabu kwa Ushirikiano na MAK Solutions ,Mpunguzi Dodoma


Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma baada ya hafla ya makabidhiano ya vitabu 200 vya kiada na ziada venye thamani ya Tsh Milioni 1 vilivyotolewa na kampuni ya MAK Solutions Ltd kuadhimisha siku ya watoto duniani
Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani


Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.


Doris akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
Miss central Zone 2014 Doris Mollel akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma
 Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu mambo yaliyomo kwenye kitable cha ‘WATER’
 Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya
Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.

Na Mwandishi Wetu,
Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.

Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo
mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.

Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana.

Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi
manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad