Mfuko wa Jamii na Maendeleo :Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yafanya ziara katika Miradi mitatu ya NSSF jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


31 Oct 2014

Mfuko wa Jamii na Maendeleo :Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yafanya ziara katika Miradi mitatu ya NSSF jijini Dar

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mbunge jimbo la Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Salum Barhan akifatilia kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni iliyokuwa ikitolewa na Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (hayupo pichani)
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyovu Mkoani Kigoma,Mh. Albert Obama akiuliza swali kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo kuhusiana na mradi huo wa Daraja la Kigamboni.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa nne kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Waheshimiwa wakijadiliana wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
 Ubao wa Maelezo ya Mradi wa Kijiji
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 
Mh. Maua Daftari
Mh. Sugu.
Baadhi la Majengo ya Mradi wa Kisasa wa Dege eco Village yakiendele kujengwa.
Picha ya pamoja ya Wabunge Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) mara baada ya kumalizika kwa ziara.Picha zote na Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad