MATUKIO :RAIS WA ZANZIBAR KATIKA SWALA NA BARAZA LA EID EL HAJJ KITAIFA MKOANI PEMBA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Oct 2014

MATUKIO :RAIS WA ZANZIBAR KATIKA SWALA NA BARAZA LA EID EL HAJJ KITAIFA MKOANI PEMBA


 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na wananchi katika swala ya Eid El Hajj iliyofanyika Kitaifa mkoani Pemba na  kuswalishwa na Sheikh Ali Kasiim Haji katika uwanja wa mpira Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba .
 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi baada ya kuswali nao pamoja swala yan Eid el Hajj katika uwanja wa Mpira jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mashekhe katika ukumbi wa Skuli ya Chwaka Jimbo Tumbe Mkoa wa kaskazini Pemba.
 Mke wa Rais wa zanzibar Mama Manamwema Shein akifuatana na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis alipowasilimkatika viwanja vya Skuli ya Kiislamu ya Kiuyu Kaskazini Pemba palipofanyika sherehe za Baraza la Eid el Hajj .
 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisimama kupokea slamu ya Heshma ya Gwaride maalum katika shrerehe za baraza la Eid el Hajj iliyotolewa na Kikosi chs Jeshi la Polisi FFU katika Viwanja vya Skuli ya Kiislamu Kiuyu kaskazini Pemba.
 Mke wa Rais wa zanzibar Mama Manamwema Shein(katikati) Mama Fatma Karume (wa pili kushoto) Mama Asha Suleiman (kushoto) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary (kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (wa pili kulia) wakiwa katika Baraza la Eid el Hajj lililofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Kiuyu Kaskazini Pemba.
 Viongozi wakimsikiliza Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na katika sherehe za sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Kiuyu Kaskazini Pemba.
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  akizungumza na Viongozi mbali mbali wananchi na waislamu katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Kiislamu Kiuyu Kaskazini Pemba.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad