MATUKIO: MISS TANZANIA 2014 , BI. SITTI ABBAS MTEMVU AAMUA KUJIVUA TAJI MWENYEWE - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Oct 2014

MATUKIO: MISS TANZANIA 2014 , BI. SITTI ABBAS MTEMVU AAMUA KUJIVUA TAJI MWENYEWE


Habari tulizozipata hivi punde kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Miss Tz 2014 Sitti Abbas Mtemvu ameandika Kujivua Taji hilo la Miss Tz 2014 kutokana na anachokiita yeye kusakamwa, kusemwa na wadau mbalimbali wa urembo na Watanzania kwa ujumla kutokana na Kudanganya Umri kitu ambacho ni kinyume na taratibu za mashindano hayo ya urembo Nchini..

Tunaendelea Kufuatilia habari hii kwa kina kuweza kufahamu kama ni kweli amejivua taji hilo maana ukishangatwa na Nyoka hata Jani likikugusa unashtuka sasa inawezekena kaamua kuandika hivyo ili kuudanganya tena Umma wa watanzania ili apate likizo ya kutokuchunguzwa na BASATA mara baada ya Idara hiyo kupewa maelekezo ya Kumchunguza na kupumzika kwa Maneno ya Watanzania ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupaza sauti ambayo kiukweli Imeonyesha kuwa Miss Tz 2014 alidanganya Umri wake. Credit Josephat Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad