MICHEZO KIMATAIFA : RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AAHIDI KUREJESHA HADHI YA MBIO ZA MAGARI (SAFARI RALLY) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


12 Sept 2014

MICHEZO KIMATAIFA : RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AAHIDI KUREJESHA HADHI YA MBIO ZA MAGARI (SAFARI RALLY)


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akiwa ndani ya gari la mmoja wa washiriki wa Safari Rally baada yake kuzindua mbio hizo uwanja wa KICC, Nairobi Septemba 12, 2014. Picha/PSCU 
Na JABRIL ADAN na JOHN KIMWERE


Kwa Mukhtasari
Rais Uhuru Kenyatta, ameahidi kufufua mbio za magari za kila mwaka za Safari Rally kuhakikisha zinarejea kwenye kalenda ya mbio za kimataifa za magari duniani. “Safari Rally imeiletea taifa hili sifa tele, kwa sasa hakuna kupoteza muda wowote lazima kuirejeshe hadhi yake," akasema.
 
RAIS Uhuru Kenyatta, Ijumaa alisema serikali itafanya juhudi kuhakikisha washiriki wa mbio za Safari Rally wamerejea kufuzu kushiriki kampeni za mataji ya dunia. Aidha alisema serikali yake itatoa ufadhili kwa washiriki wa mbio za Safari Rally kuwafanya wafurahie kushiriki katika mbio hizo.
“Tunataka kurudisha mbio hizo katika kiwango zilizokuwa hapa nyuma kiasi cha kuwapa washiriki wazo furaha tele hasa kufuzu kushindania mataji makuu duniani,” alisema. Rais alisema haya kwenye ukumbi wa kitaifa wa KICC alipozindua mashindano ya KCB Safari Rally makala ya 62.

Aidha rais Kenyatta alisema, mbio za Safari Rally zimekuwa maarufu kwa muda mrefu katika miaka ya hapa awali kwenye kalenda ya michezo duniani. “Safari Rally imeiletea taifa hili sifa tele, kwa sasa hakuna kupoteza muda wowote lazima kuirejeshe hadhi yake.”
Mbio hizo zilikuwa kwenye kalenda ya mashindano ya kimataifa hadi 2003 pale zilizoondolewa kutokana na maandalizi mabaya na mipango duni.
Rais alipeperusha bendera ya taifa kwa magari matatu ya kwanza na kuwatakia washiriki heri njema kwenye kampeni za mashindano hayo. Aidha alitoa mwito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi kutazama mbio za magari hayo na kuchukua tahadhari kuzuia kutokea kwa ajali.
“Nawaomba watazamaji kuunga mkono mchezo huu, lakini kuwa makini raha isiwazidi kusudi kuzuia kutokea kwa ajali,” alidokeza. Rais alitoa mwito kwa wazazi kuhakisha usalama kwa watoto wao kwenye barabara zitakazotumika na washiriki mbio hizo.

Usalama
Mbio za Safari Rally ni mchezo maarufu kwa muda mrefu ambapo Kenya imekuwa ikishiriki mapambano ya viwango vya haiba kubwa duniani. Mwanzilishi wa taifa hili, Jomo Kenyatta aliweka historia mwaka 1968 kwa kuzindua mchezo wa kimataifa kwa mara ya kwanza.
Gavana wa Kaunti ya Nairobi, Evans Kidero akizungumza kwenye hafla ya Ijumaa alishauri watazamaji kufurahia mchezo huo na kuhakikisha usalama wao. Waziri wa usalama wa Ndani, Joseph Ole Lenku aliyewakilisha Waziri wa Michezo, Hassan Wario pia alizungumza kwenye hafla hiyo. Chanzo :Taifa Leo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad