Mapishi ya Leo; NA Chef Kile: Kuunga Dagaa kwa Nazi – Kisha Kula kwa Ugali - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Sept 2014

Mapishi ya Leo; NA Chef Kile: Kuunga Dagaa kwa Nazi – Kisha Kula kwa Ugali






Katika mapishi ya leo ni namna ya kuunga dagaa kwa nazi na kufanya mboga iwe tamu haswaaa.

MAHITAJI
  • Dagaa ( Kiasi ya kutosha watu wanne)
  • Kitunguu maji kimoja
  • Souse ya nyanya ( Endelea kusoma utaona maelezo juu ya hii)
  • Karoti moja au mbili
  • Tui moja la nazi ( Liwe tui zito)
Kwanza pata maelezo juu ya souse
Mimi huwa naandaa souse ya nyanya ambayo huwa inafaa kwa matumizi ya kuunga mboga mbali mbali – na ndio hiyo souse naizungumzia . Hata wewe waweza andaa na kisha ukaweka kwa friji ukawa unachukia kiasi unachohitaji wakati wa mapishi yako.
Jinsi ya kuandaa – MAHITAJI sasa hapa nitakupa kwa ujumla maana siwezi jua wewe utaandaa souse kiasi gani
  • Nyanya za kutosha
  • Vitunguu Maji
  • Vitunguu swaumu
  • mafuta ya kula ( vegetable oil)
  • Binzari
  • Pilipili Manga
  • Mixed Herbs
  • Mustard
  • Chumvi
  • Supu ya kuku au nyama ya ngome ( kwa wingi)
Kuandaa – Maandalizi ni ya kawaida tu – Weka vitunguu maji katicha chombo chako na mafuta anza kuunga kisha weka vitunguu swaumu , binzari, pilipili manga, mixed herb, chumvi,mustard,endelea kuunga na vikiwa vyaelekea kubadili rangi weka nyanya zako sasa kisha weka na ile supu kwa wingi tu kisha acha ichemke kwa mda mrefu hadi maji yaishe kabisa ibaki souse nzito. Hapo ni tayari iache ipoe kisha hifadhi katika friji kwa matumizi kila mara utakapo hitaji. – Souse ikiwepo inasaidia wewe kuandaa mlo kwa mda mfupi sana.
SASA TUENDELEE NA DAGAA ZETU
Andaa dagaa wako tayari kwa mapishi – Waoshe vizuri na maji moto kabisa , hakikisha hawana mchanga, wakaushe kwa jua au kwa oven – pale unapoona panakufaa.
kuunga dagaa kwa nazi 
Weka chombo katika moto kile ambacho utatumia – weka mafuta kiasi na uweke kitunguu – kitunguu kikiwa kimeiva bila kubadilika rangi weka wale dagaa wako. Endelea kuwaunga unga hapo kisha weka karoti zako hapo pamoja na ile souse yako. Ongeza maji kidogo kisha funika ichemke kwa dakika 3-4 , ili dagaa walainike kidogo na maji yapungue. Kisha weka lile tui lako la nazi; koroga kwa muda hadi liwe tayari na hii huwa ni dakika 2-3.
Sasa toa mchuzi wako wa dagaa maana hapo ni tayari na ni nzuri kula na ugali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad