ELIMU YETU : SHULE YA MSINGI YOMBO YAPEWA MSAADA WA MADAWATI YENYE THAMANI YA MILIONI 10 NA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE (TAA) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Aug 2014

ELIMU YETU : SHULE YA MSINGI YOMBO YAPEWA MSAADA WA MADAWATI YENYE THAMANI YA MILIONI 10 NA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE (TAA)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan Said Suleiman (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Eva Mbena.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan Said Suleiman (katikati), akipeana mkono na dada mkuu wa shule hiyo, Celina Dismas baada ya kukabidhi madawati hayo. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo Emanuel Mlangali (kulia), akiwa na walimu wa Shule jirani. Kutoka kushoto ni Mwalimu Saum Mwabi wa Shule ya Msingi Mwale na Mwalimu Anna Kyoma.

Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. 
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Christina Kasyupa akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kuimba kwenye sherehe hiyo.
Kikundi cha Makhirikhiri cha shule hiyo kikitoa burudani.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan Said Suleiman akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo.


Dotto Mwaibale wa mtandao wa www.habari za jamii.com

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imetoa msaada wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na changangamo ya madawati shuleni hapo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo Dar es Salaam leo aasubuhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Suleimkan Said Suleiman alisema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya TAA kwa shule hiyo walioitoa mwaka jana.

"Kazi hii tunayoifanya ni kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa na kudumisha ujirani mwema uliopo kati ya shule yenu na Kiwanja cha chetu cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)" alisema Suleiman.

Alisema mwaja jana TAA ilitoa ahadi kwa shule hiyo ya kuwapa sh.milioni 10 ili ziwezekusaidia kupunguza tatizo la madawati ahadi ambayo wameitimiza jana kwa kutoa madawati hayo yenye thamani ya sh.milioni 10.

Suleiman alisema msaada huo utakuwa kwa kamati ya shule hiyo na kuongeza jitihada za kuboresha zaidiufaulu kwa shule hiyo na wanafunzi kuhudhuria shuleni bila ya kukosa kwa faaida yao na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Suleiman alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa shule hiyo pamoja na wanafunzi hao kuyatunza madawati ili yaweze kusaidia na vizazi vingine.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Christina Kasyupa aliishukuru TAA kwa msaada huo kwa shule hiyo na kuwa wameupata kwa wakati muafaka kutokana na changamoto waliyokuwa nayo ya ukosefu wa madawati.

Shule ya Msingi ya Yombo ilianzishwa mwaka 1962 na imefanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 85 kwenda sekondari mwaka2013 na kupata cheti cha ugaguzi daraja A na sasa ipo katika Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad