WANAWAKE NA MAENDELEO :MALKIA NOMSA MATSEBULA WA SWAZILAND AZURU TANZANIA KWA MWALIKO WA MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Jul 2014

WANAWAKE NA MAENDELEO :MALKIA NOMSA MATSEBULA WA SWAZILAND AZURU TANZANIA KWA MWALIKO WA MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE.

 Malkia wa Swaziland Mheshimwa Nomsa Matsebula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Ndugu Nurdin Babu mara baada ya helikopta iliyomchukua kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati huko wilayani Rufiji ambako alikwenda kutembelea Shule ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA. Tarehe 2.7.2014. Kulia ni Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.

 Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama Dkt. Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kuwasili huko Nyamisati
 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa amefuatana na mwenyeji wa Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamisati waliofika kumlaki mara baada ya helikopta iliyomleta kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati
 alkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akionyeshwa namna wanavyotumia I-pad katika baadhi ya masomo yao hapo shuleni Wamanakayama na mwanafuzi Rehema Shao aneyesoma kidato cha pili huko mwanafunzi Asia Idd (kushoto) akisubiri zamu yake.
 Mwanafunzi Assia Idd akimwonyesha Malkia Matsebula kutoka Swaziland namna ya kutumia i-pad kwenye masomo ya sayansi na hesabu wakati Malkia huyo alipotembele Shule ya Sekondari ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula wakitembelea maeneo mbalimbali ya shule ya Wamanakayama
 Mwanafunzi Elizabeth Kipoto anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Wamanakayama akiwaonyesha wageni jaribio la kujua kama kuna protini kwenye vyakula katika maabala ya Biologia shuleni hapo
 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akipanda mti wa kumbukumbu ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati katika wilaya ya Rufiji.
 Mgeni akipanda mti
 Wimbo wa taifa
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni wake Malkia Matsebula wa Swaziland kuongea na wanafunzi na wafanyakazi wa Shule hiyo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni wake Malkia Matsebula wa Swaziland kuongea na wanafunzi na wafanyakazi wa Shule hiyo.
  Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
  Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
  Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Wamanakayama baada ya kuitembelea shule hiyo
 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa na mwenyeji wake Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi na viongozi mbalimbali.
 Mke wa Mama Salma Kikwete akimpokea Mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebulan wakiongea na wanahabari
 Mke wa Mama Salma Kikwete akimpokea Mgeni wake Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula mbele ya jengo la ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Malkia Nomsa Matsebula na Mama Hulda Kibacha, Mjumbe wa Bodi ya WAMA (Kulia kwa Malkia), na His Royal Highness Prince Muvela (kulia) na His Royal Highness Prince Sicalo (kushoto).

  Malkia Matsebula na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza Afisa Uragibishi na Mawasiliano wa WAMA Ndugu Philomena Marijani  akitoa maelezo juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.
 Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake zawadi ya picha.
 Mama Salma Kikwete akimkabidhi Malkia Matsebula zawadi ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa Tanzania.
 Malkia Nomsa Matsebula akimkabidhi Mama Salma Kikwete mchango wake wa dola 3000 kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama.

 Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akizungumza na Mama Anna Mkapa wakati wa futari ambayo iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Ikulu 
 Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa futari aliyomwandalia Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula anayetembelea Tanzania  huko Ikulu 
Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiongea na viongozi wanawake mbambali waliohudhuria futari  aliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Ikulu. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad