RIADHA NCHINI : GIDABUDAY ASEMA " Glasgow: BMT na RT wametupotezea medali zetu watanzania, wamlaghai JK " - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Jul 2014

RIADHA NCHINI : GIDABUDAY ASEMA " Glasgow: BMT na RT wametupotezea medali zetu watanzania, wamlaghai JK "


 
Siku ya kuagwa timu ya Tanzania ya Jumuiya ya Madola rais Jakaya Kikwete hakutaarifiwa kwamba viongozi wa RT walichaguliwa kinyume cha katiba na pia kinyume cha sheria # 12 iliyotungwa na bunge 1967.

Lakini pia waziri Bernard Membe amejikuta akitoa pesa za watanzania kwa wahuni waliodharau katiba ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. Ningepata wasaa wa kumuuliza waziri Membe ningemuuliza kwamba 'Ni kwa nini hakusumbuka kupeleleza uhalali wa RT'?

Hata hivyo nampa pongezi hili 'Thanks BUT no thanks Hon. Membe' kwa kuwa ametoa pesa ambazo zilitumika kubagua wanamichezo sababu wanariadha waliokwenda kambi za nje HAWAKUSHINDANISHWA na wenzao ili kubaini nani bora atakayeweza kuiletea Tanzania medali.

Kwa maana nyingine waziri ameshiriki kubariki RT kubagua uwepo wa wanawake katika timu ya riadha ya taifa 'Ama kwa kujua ama bila kujua'

Kenya kwa siku ya jana tu wamekusanya medali TANO, Uganda nao wamenyakua medali lakini sisi tunamdanganya rais wetu!  

"HONGERA NYAMBUI KWA KUFANIKIWA KUMLAGHAI JK, WE MKALI UNAOGOPWA HADI NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad