MATUKIO :MHE. PETER MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Jul 2014

MATUKIO :MHE. PETER MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

 Maafisa wa Ubalozi, Bwana Amos Msanjila na Dada Caroline Chipeta, Wakimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Pinda na Mkewe (Mama Tunu Pinda) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Peter Pinda akipokewa, kukaribishwa na kusalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Uingereza.

 Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano wao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda, alikutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai 2014, mara baada ya ziara yake fupi ya kikazi nchini humo.

Mkutano huo na Watanzania ambao uliofanyika Ubalozini, Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa taarifa mbalimbali za maendeleo nchini, hususan mchakato wa Katiba mpya, sera ya Diaspora na maandalizi ya chaguzi mbalimbali zinazokuja. Mkutano huo ulimalizika kwa maswali na majibu na baadae wananchi kupiga picha na Waziri Mkuu kama inavyoonekana kwenye picha hizi hapo chini.
 Watanzania waliofika kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda katika mkutano huo.
 Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania, wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, alipokutana na kuzungumza nao
 Mke wa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akiongea na Watanzania waliofika kwenye mkutano wao na Mhe. Waziri Mkuu.
 Mhe. Waziri Mkuu na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad