MAPISHI, Na Chef Kile : Mapishi ya leo ni Pizza ya kuku – Kinyumbani zaidi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Jul 2014

MAPISHI, Na Chef Kile : Mapishi ya leo ni Pizza ya kuku – Kinyumbani zaidi









Haya tena leo tunapika pizza ya kuku – ni mlo mtamu sana sana na wafaa kuliwa mida ya mchana
MAHITAJI
  • Unga tayari wa pizza (Pizza dough)
  • Souse kwa ajili ya pizza
  • Cheese ( Pizza topping)
  • Nyanya moja
  • Nyama ilokwisha chemshwa ya kuku ila ni minofu tu
Sasa Kabla ya kutiririka na namna ya kuiweka pizza yako labda nikueleze kidogo namna ya kuandaa unga wa pizza
Utahitaji
  • Unga wa ngano nusu kilo
  • Mafuta ya kula (vegetable oils) zaidi ni Olive oil ndio inafaa – kiasi cha nusu kikombe
  • Amira pakiti moja ( Kijiko kimoja cha chakula)
  • Sukari kijiko kimoja
Sasa kwanza andaa amira yako kwa kuumua weka katika chombo na maji kidogo (Kiasi ya nusu kikombe) yawe ya vuguvugu mimina amina na ile sukari kisha acha kwa dakika 5 ili kuumua. Baada ya amira kuwa tayari mimina mafuta katika ule unga na hiyo amira kisha anza kuukanda unga wako kwa dakika zisizo pungua 20 …. baada ya hapo unga utakuwa tayari. Sasa unga wa pizza huwa hautumiki mara tu baada ya kuwa tayari bali unauaacha kwa  mda usiopungua masaa mawili na kuendelea ndipo unakuwa tayari kwa matumizi.
Jinsi ya kuandaa Souse ya pizza
Hii ni rahisi tu sema unahitaji nyanya kwa wingi. Unga kama mboga hivi ila hii ni ya nyanya
Unahitaji
  • Nyanya 10
  • Vitunguu 2
  • Mustard kavu vijiko viwili ya chai
  • Mixed herb
  • Pilipili Manga
  • Chumvi
  • Supu ya kuku
Tengeneza souse yako kwa kutumia  hayo mahitaji…
Baada ya kuwa ushaweka mahitaji yako sawia pasha jiko lako moto vizuri sana. Kata unga ule wa pizza kiasi unachohitaji sukuma na kupata saizi ya kutosheleza chombo chako. Pakaa butter katika chombo ili isije shika chini. Kisha weka .
Weka hiyo chapati yako na uweke souse ipake juu ya chapati pote kisha weka nyama nyama zile za kuku na kisha weka ile cheese ( Pizza topping) , weka zile slices za nyanya na weka tena souse kidogo.
pizza ya kuku kinyumbani
Weka katika jiko kwa dakika 10 baada ya hapo itakuwa tayari kwa kula

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad