JAMII ZETU :YATIMA KITUO CHA MWANDALIWA WAWEZESHWA KUANZISHA MRADI WA KUJIPATIA KIPATO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Jul 2014

JAMII ZETU :YATIMA KITUO CHA MWANDALIWA WAWEZESHWA KUANZISHA MRADI WA KUJIPATIA KIPATO


  Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es salaam. Vodocom ilitemebela kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondeshwa na kituo hicho. 
 Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Jamii wa Vodafone Laura Turkington akiwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Mwandaliwa wakifurahia picha kupitia simu ya mkononi ya Laura. Wafanyakazi wa Vodacom  walitembelea kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondehswa na kituo hicho
 Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano ya Vodacom Rosalyn Mworia akigawa vitabu vya kujifunzia mambo mbalimbali vilivyochangwa na wafanyakazi wa Vodacom kusaidia watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa. Mbalina vitabu na vifaa vya kuchezea, Vodacom Foundation nayo ilikabidhi Sh 20 Milioni kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.
 Mkurugenzi wa Kituo cah mwandaliwa Islami cha Bunju jijini Dar es salaam Halima Ramadhan akiipitia kwa umakini mfano wa hundi mara baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa Vodacom. Fedha hizo zimetolewa na Vodacom Foundation   kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Mariam Abdallah akiwafundisha kusoma baadhi ya watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwemo pia  vitabu. Mbali na vitu hivyo, wafanyakazi ho walikabidhi hundi ya Sh 20 Milioni iliyotolewa na Vodacom Foundation kusiadia mradi wa ushonaji na ufugaji kituoni hapo.
 =======  =======  =======
Yatima Kituo cha Mwandaliwa wawezeshwa kuanzisha mradi wa kujipatia kipato
Dar es Salaam, Julai 1, 2014 … Kituo cha Kiislamu cha kulelea watoto yatima na ushauri  cha Mwandaliwa Islamic Orphans Home and Counseling Support (MIOCA’S) kilichopo Mbweni jijini dar es salaam kimepokea Sh 20 Milioni kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji ili kujijenga kiuchumi.
Fedha hizo zimekabidiwa kituoni hapo wakati na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea kituo hicho kwa lengo la pmaoja na mambo mengine kuwaislisha pia Zawadi mbalimbali walizozikusanya wka ajili ya watoto wanaelelewa kituoni hapo.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo kwa niaba ya Vodacom Foundation, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Angela Mwakasege amesema Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation wakati wote inaguswa na changamoto zinazoizunguka jamii ikiwemo suala la watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu.
Amesema hatua ya kukabidhi fedha hizo pamoja na zawadi za vitabu na vifaa mbalimbali vya kuchezea watoto ni kielelezo cha jinsi ambavyo wafanyakazi na kampuni kwa ujumla inayoguswa na kusukumwa kusaidia jamii na kuweka mbele ajenda ya kusaidia kukabiliana na changamoto hizo
“Leo tunafuraha sana kufika hapa, tunawapenda sana na tunaimani kwamba hiki tunachpowakabidhi kitawasaidia kutimiza lengo lenu la kujijengea uwezo wa kiuchumi kupitia miradi mnayokusudia kuianzisha ya ushonaji na ufugaji.”Alisema Mwakasege
“Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Vodacom kipekee tunawpongeza sana walezi na viongozi wa kituo hiki kwa namna mlivyokubali kujitoa kuwalea watoto hao. Sisi tunatambua kuwa hiyo sio kazi rahisi, tunawatia moyo mzidi kujitoa kwa ajili ya akzi hii.”Alisema 
Kituo hicho chenye watoto 94 kinatarajia kuanzisha miradi ya ushonaji na ufugaji itakayotumika kukiwezesha kituo kuwa na vyanzo vya mapato na pia kuwa na fursa ya kuwajengea uwezo wa stadi za kazi na kujiajiri watoto ili kuwapa uwezo wa kujitegemea katika siku za usoni.
Kwa sasa kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea misaada ya wahisani mbalimbali, lakini kuanzishwa kwa mradi huo wa ufugaji kuku wa nyama na ushonaji kutawezesha kituo hicho kuounguza utegemezi wa wahisani.
Akisoma maelezo ya kituo na shukrani kwa Vodacom Foundation na wafanyakazi wa Vodacom kw akile walichowawezesha, Katibu wa kituo hicho Omary Ramadhan amesema watoto walio wengi hupatikana kwa kuletwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni na husomeshwa na wengi wao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia ya chekechea.
Akizungumzia msaada huo, xx alisema “ Tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu na baadae kukubalika kwa ombi letu ka kusaidia fedha kufadhili mradi wa ufugaji na ushonaji. Tunajua haikuwa kazi nyepesi, tulihataji kuwa wavumilivu lakini hatiame tuanshukuru sana kuona leo tunaelekea kutimzia ndoto yetu ya kuwa na miradi ya kiuchumi.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad