MATUKIO :DKT GHARIB BILAL AONGOZA SWALA YA IDDI KITAIFA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM LEO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Jul 2014

MATUKIO :DKT GHARIB BILAL AONGOZA SWALA YA IDDI KITAIFA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi,Dkt. Hussein Mwinyi (katikati) akijumuika pamoja na Waumini wenzake wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
 Masheikh mbali mbali wakiwa kwenye ibada hiyo.

 Umati wa Waumini wa Kiislam ukiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo,tayari kwa kushiriki ibada ya Eid El Fitr.
Wakinamama pia walijitokeza kwa wingi wao kwenye Ibada hiyo.
Watangazi wa TBC Taifa wakiongozwa na Maalim Sued Mwinyi wakirusha matangazo live.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akipeana mkono wa Eid na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam mara baada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal (nyuma ya Shehe anayeswalisha) akijumuika na waumini wa Kiislamu kwa Swala ya Iddi Kitaifa iliyofanyika katika Bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad