BARABARA ZETU : JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Jul 2014

BARABARA ZETU : JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.Picha Zote Na Dj Sek Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad