MAPENZI KWELI YANAUA : MWANAFUNZI AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA VISU NA MPENZI WAKE MBELE YA WAZAZI WAKE - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Apr 2014

MAPENZI KWELI YANAUA : MWANAFUNZI AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA VISU NA MPENZI WAKE MBELE YA WAZAZI WAKE


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
SIRI nzito ya mauaji ya kinyama ya mwanafunzi wa Chuo cha Savanna Bridge cha jijini Arusha, Winfrida Akunay (18) aliyechomwa kisu mara sita eneo la shingo na kifua mbele ya baba yake mzazi imegundulika, Amani linakupatia.
Winfrida Akunay (18) enzi za uhai wake.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, mtuhumiwa wa mauaji hayo, Robert Isaac (22) alitimiza ukatili huo nyumbani kwa baba wa marehemu Majengo Juu jijini hapa, Machi 25, mwaka huu, saa 2:12 usiku.
Ishu kubwa iliyojitokeza ni wivu wa mapenzi ambapo mgogoro mzito uliibuka kwa wawili hao.

Gazeti hili lilifuatilia kwa makini sakata la mauji hayo na kufanikiwa kupata waraka wa siri ulioandikwa na mtuhumiwa huyo ambapo sehemu ya waraka ilisema:
Mwili wa Winfrida Akunay ukiwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi.

"Nakupa wiki moja ya kufikiria, kama utaendelea na msimamo wako wa kutokuwa na mimi nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe na mimi kujiua." Mwenyekiti wa Mtaa wa Remtula, Majengo alisema baada ya mauaji hayo kesho yake walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa eneo la Ngusero alipokuwa akiiishi na mjomba wake na kufanya upekuzi chumbani ambapo walikuta karatasi iliyoandikwa:

"Mimi Robert Isaac nikiwa na akili timamu, nilikuwa na marehemu Winfrida kama wachumba kwa muda wa miaka miwili iliyopita, tuliahidiana kuoana baada ya kula yamini ya damu, lakini ilipofika mwezi wa pili, mwaka huu, marehemu alinikataa, lakini mwezi wa tatu tulifanikiwa kurejesha mahusiano mara tatu.”
Mwili wa Winfrida Akunay ukiombewa kabla ya kwenda kuzikwa.


Unaendelea: ‘’Baadaye ndani ya mwezi huohuo, marehemu alibadilika na
kuniambia hanitaki tena, nilimpa wiki moja afikirie na kubadilisha msimamo wake huku nikimkumbusha juu ya kiapo chetu cha damu kwamba kifo kitutenganishe.’’

Waraka huo unaendelea: ‘’Nilimwambia kama hutabadili msimamo wako
nitakuua kwa mikono yangu miwili na kisha nami kujiua, nimemwachia mdogo wangu shamba na baadhi ya vitu vyangu akabidhiwe yeye.”
Mwili wa Winfrida ukiombewa.

Akizungumzia mauaji hayo, baba mzazi wa marehemu, Paul Akunay (59) ambaye alilazwa katika Hospitali ya Kanisa Katoliki, Saint Elizabert jijini hapa baada

ya kujeruhiwa kwa kisu mguuni na mkononi wakati akimwokoa mtoto wake, alisema:
“Siku ya tukio mtuhumiwa alifika nyumbani majira ya saa 2 usiku na kumtaka binti yangu wazungumze walau kwa dakika moja, nilimweleza aondoke.
“Mtuhumiwa aligoma kuondoka, badala yake alisonga mbele hatua moja akimwelekea marehemu alipokuwa amekaa kisha akachomoa kisu kwenye koti na kumchoma marehemu shingoni.
Mazishi ya Winfrida Akunay.

Nilijaribu kumshika lakini nilijikuta nikishika makali ya kisu na kunijeruhi mkono wa kushoto na baadaye alinichoma mguuni, nikamwachia ambapo alimrudia mwanangu na kuendelea kumchoma zaidi ya mara sita kifuani na shingoni akirudiarudia. Alifanikiwa kukimbia.

Mzee huyo alidai hakuwahi kumwona kijana huyo hata siku moja na siku hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza na wala hatambui uhusiano wake na marehemu.
Marehemu Winfrida alizikwa kijijini kwao, Makuyuni wilayani Monduli, Arusha, Machi 29, mwaka huu. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi bado wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.
GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad