JIJI LETU ARUSHA: MIUNDOMBINU YA BARABARA INAFANYIWA UKARABATI ,ILA SEHEMU ZINGINE BADO KUNA CHANGAMOTO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Apr 2014

JIJI LETU ARUSHA: MIUNDOMBINU YA BARABARA INAFANYIWA UKARABATI ,ILA SEHEMU ZINGINE BADO KUNA CHANGAMOTO

 Hii ni barabara ya Arusha -Nairobi road, mitaa ya Technical ambayo ina fanyiwa ukarabati wa upanuzi ili kuruhusu kupishana kwa magari makubwa ya mizigo na mgari ya kawaida.

Pia itaruhusu kuwekwa kwa taa za kuongozea magari ambayo yatawekwa makutano ya Moshi-Arusha Road na Nairobi road karibu na Triple A na Arusha Technical College.
Mitaa ya Technical College kuelekea triple A
 ukarabati umefanyika pande zote mbili za barabara.
 Hii ni barabara ya Sombetini-Ngusero Road, nayo inafanyiwa ukarabati kwa kiwango cha lami kutoka soko mjinga hadi kona ya Sombetini. 
 Hii ni barabara ya OLASITI ambapo inakabiliwa na changamoto nyingi, kwa mfano ; hakuna mitaro ya kupelekea maji, hakuna magari ya abiria inayofika huko ingawa kuna magari ya abiria (hiace) imeandikwa Stand-Olasiti lakini haziendi huko zinanyookea kwa-moromboo, kina mama wanapata shida ya kubeba mizingo yao kupeleka sokoni wanatembea zaidi ya kilomita 3.
Blogu ya Wazalendo 25 Blog ilitembelea mitaa ya Olasiti na kujionea adha wanayoipata jamii ya eneo hili. Mamlaka husika imehaswa kutatua kero hizi za barabara na matatizo mengine ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad