AJALI MBAYA YATOKEA : BASI LA URIO SAFARIS LAPATA AJALI MAENEO YA K.I.A 31 WAJERUHIWA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Apr 2014

AJALI MBAYA YATOKEA : BASI LA URIO SAFARIS LAPATA AJALI MAENEO YA K.I.A 31 WAJERUHIWA

 wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea jana jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruhiwa


 Basi aina ya Urio Safaris yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea  leguruki mkoani  Arusha jana limepinduka katika eneo la kia na kujeruhi watu zaidi ya 31

kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani

"dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama barabara ndipo ilipo anguka ghafla  na kupinduka mara tatu, hapa unavyoiona tumeigeuza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina

mpaka kamera ya Wazalendo 25 Blog inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwisha pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya pasaka .
 picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye  basi hilo aina ya Urio Safaris lililopata ajali jana jioni katika eneo la Kia wilayani Hai  mkoani Kilimanjaro
Picha na Woinde Shizza wa blogu ya Wazalendo 25 Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad