RIADHA TANZANIA BADO NI "DHAIFU" : WAKENYA WAPETA KATIKA MBIO ZA KILL MARATHON, MOSHI KILIMANJARO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Mar 2014

RIADHA TANZANIA BADO NI "DHAIFU" : WAKENYA WAPETA KATIKA MBIO ZA KILL MARATHON, MOSHI KILIMANJARO

Mshindi wa kwanza wa Full Marathon David Ruto akionesha mfano wa hundi ya sh. mil 4 iliyotolewa kwa mshindi wa kwanza.






MTANZANIA Jackline Sakilu amewatuliza Watanzania kwa kuibuka mshindi katika mbio za mwaka huu za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon.

Sakilu ambaye anatokea katika Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ), amefanya hivyo jana katika mbio za Kilomita 21 wanawake, akikimbia kwa muda wa saa 1:12:43 mbele ya wanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya.


Katika nafasi ya pili alikuwa ni mwanariadha Cynthia Towett, aliyekimbia kwa muda wa saa 1:14:33, na katika nafasi ya tatu alikuwa ni Naomi Maiyo aliyekimbia kwa muda wa saa 1:17:47 wote kutoka Kenya.

Katika mbio hizo kwa upande wa wanaume, nafasi ya kwanza alikuwa ni Alfred Lagat kutoka Kenya ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:02:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Silah Limo (1:03:04) na Keneth Kandie (1:03:20) huku Mtanzania wa pekee katika kumi bora, Alfred Felix, kutoka Klabu ya riadha ya Holili (HYAC) akishika nafasi ya tano (1:03:27).

Wakati huo huo zimwi la kufanya vibaya katika mbio ndefu (Kilomita 42) imeendelea kuiandama Tanzania baada ya Wanariadha kutoka Kenya kutawala mbio hizo kwa mwaka mwengine tena.

Katika Mbio za wanaume, Mshindi  wa  kwanza David Ruto kutoka Kenya aliyetimua mbio hizo kwa muda wa masaa 2:16:04,nafasi ya pili alikuwa ni Julius Kilimo (2:16:17) na nafasi ya tatu ikishikwa na Victor Serem 2:16:32 huku Mtanzania wa kwanza katika mbio hiozo kwa upende wa wanaume, Daudi Lwabe, akiingia katika nafasi ya nane akitumia muda wa masaa 2:18:34.

Katika upande wa wanawake mshindi alikuwa ni Frida Lodera aliyetumia muda wa masaa 2:40:11, nafasi ya pili ni Joan Rotich aliyetumia muda wa masaa 2:42:46 na nafasi ya tatu ikashikwa na Abigal Toroitich ambaye alitumia muda wa masaa 2:55:14 ambapo Mtanzania pekee aliyeingia kumi bora, Banuelia Bryton,  akiingia katika nafasi ya tisa kwa kutumia muda wa masaa 3:12:26.

WATANZANIA WAENDELA KUFANYA VIBAYA.
Pamoja na waandaaji wa mbio hizo kuendelea kutoa ahdi nyingi za kuongeza zawadi kwa washindi wazalendo, wanariadha wazawa wameendelea kufanya vibaya katika mbio hizi.

Katika mbio za mwaka huu, wanariadha kutoka nchi jirani wameendelea kuonesha umwamba katika riadha hasa mbio ndefu mbeloe ya watanzania tofauti na ilivyo katika miaka ya 70 enzi za akina Filbert Bayi na Suleiman Nyambui.

Kutokana na matokeo ya mbio za mwaka huu, nafsi zote za juu, nafasi ya kwanza hadi ya tano, tofauti na mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanawake uliochukuliwa na Jackline Sakilu, mbio zote zilitawaliwa na wakenya huku Watanzania wakilazimika kushika za nafasi ya tano, nane na tisa.

WAZIRI MUKANGARA AAGIZA RT KUANZA MAANDALIZI MAPEMA KUFUTA UTEJA.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara ameitaka chama cha Riadha Tanzania (RT), kuhakikisha inaweka mikakati mizuri ya kuwaanda wanariadha wanaoshiriki mbio za kitaifa na kimataifa ili kuwafanya kuwa tayari kuliko kusubiri hadi mashindano yafike ndipo waanze kufanya maandalizi.

Dkt. Mukangara ambaye aliokuwa mgeni Rasmi katika mbio za mwaka huu Kilimanjaro marathon, aliyesema hayo katika hotuba ambapo aliwataka viongozi wa michezo riadha ikiwemo kujiandaa kikamilifu kushiriki mashindano yanayoandaliwa hapa nchini.

Alisema Wadhamini wanatumia fedha nyingi kuandaa mashindano lakini kutokana na ushiriki mbovu wa watanzania unaochangiwa na maandalizi duni, umekuwa ukiwakatisha tamaa watu wenye nia ya kuwekeza katika michezo hapa nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambao ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo kwa mwaka wa 12 sasa, George Kavishe, alisema TBL itaendelea kuhakikisha inaboresha udhamini wake katika mashindano hayo na kuendelea kuyapa sura ya kimataifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad