NDOTO ZA GIDABUDAY : TANZANIA INAHITAJI KITUO KIKUBWA CHA MICHEZO(TRAINING CENTER) ILI KIWEZE KUSHINDA KIMATAIFA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


6 Mar 2014

NDOTO ZA GIDABUDAY : TANZANIA INAHITAJI KITUO KIKUBWA CHA MICHEZO(TRAINING CENTER) ILI KIWEZE KUSHINDA KIMATAIFA

Zambia Olympic Youth Development Center

 Mwaka 2004 Tanzania ilipata bahati ya kuahidiwa kujengewa kituo kikubwa cha kisasa cha michezo (Tanzania Olympic Youth Development Center) ambayo ingegharimu USD 10million lakini viongozi wa TOC kwa kushirikiana na viongozi wasio wazalendo walikwamisha.

Kilichotakiwa na IOC ni kuhakikishiwa kwamba eneo kubwa lisilo na utata wa kisheria linapatikana ikiwa na vithibitisho vya kiumiliki ili hapo baadaye kusiwepo na utata (contradiction) za kisheria.

Bila aibu wala uzalendo kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ilihakikisha kwamba kituo hicho hakijengwi kwa sababu ya wao kuhofia masilahi yao ya upatikanaji wa tenda za kimichezo katika center zao walizojiwekezea.

Kwa mfano:  kama mtu anapata tenda ya Copa Coca-Cola ya Tsh: Bilioni kila mwaka alafu atawezaje kupata kiasi hicho cha pesa iwapo taifa litakuwa na center yake? Hivyo kigogo mmoja tu mwenye center yake alishawishi kamati nzima waikatae ofa hiyo ya IOC nao kwa akili zao ndogo wakaafiki upuuzi huo.


Hatimaye TOC ikashindwa kurudisha majibu kwa IOC ndipo IOC ikaamua kupeleka ofa hiyo Zambia na wazambia hawakuchezea nafasi hiyo na hivi sasa kuna kituo kinachoitwa Zambia Olympic Youth Development Center.

Je wizara na baraza la michezo (BMT) wamefanya juhudi gani kuwachukulia hatua watu hao?  Watu ambao kimsingi ni ‘Wahujumu Uchumi’ maana kupindisha (Divert) masilahi ya taifa ni kuhujumu uchumi wa taifa kwani watoto wengi wenye vipaji wangenufaika na kituo hicho bila gharama.

'Tutaendeleza mapambano ya mapinduzi ya kimichezo hadi pamba za masikio ya waheshimiwa serikalini zidodonke na waanze kusikia vilio vyetu'. CHANZO: gidabuday.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad