MSAADA TOKA UN-ICTR : MAHAKAMA YA HALAIKI YA WATU WA RWANDA YATOA MSAADA WA MAGARI MAWILI KWA JESHI LA POLISI,JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


8 Mar 2014

MSAADA TOKA UN-ICTR : MAHAKAMA YA HALAIKI YA WATU WA RWANDA YATOA MSAADA WA MAGARI MAWILI KWA JESHI LA POLISI,JIJINI ARUSHA

Bwana Robert Foot akikabidhi funguo za magari hayo kwa Kamanda wa mkoa wa Arusha ACP .Liberatus Sabas

 Kamanda Sabas akitoa shukrani zake kwa uongozi wa UN-ICTR kwa msaada huo. Katikati ni Afisa Habari wa Mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa 
 
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inyoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani hapo. 
 
Magari hayo ni baadhi ya yale yaliyokuwa yakitumika kwa shughuli za usalama  - kubebea watuhumiwa au watu nyeti - na mahakama hiyo inayotarajiwa kumaliza shughuli zake mwakani. Magari hayo yameimarishwa kiusalama ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake. Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Liberatus Sabas.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad