JESHI LETU MAKINI : DKT. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KAMANDO NA UHANDISI MEDANI, MKOANI MOROGORO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


5 Mar 2014

JESHI LETU MAKINI : DKT. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KAMANDO NA UHANDISI MEDANI, MKOANI MOROGORO

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.

Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad