CHADEMA ARUSHA :UKWELI KUHUSU MADIWANI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ,MJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Mar 2014

CHADEMA ARUSHA :UKWELI KUHUSU MADIWANI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ,MJINI ARUSHA


Mh. Naibu Meya Prosper Msofe ...Picha/Maktaba


Siku za hivi Karibuni Kumetokea Upotoshwaji kuhusu Madiwani wa Chadema na Nafasi ya Naibu Meya kujihusisha na Biashara jambo ambalo si la kweli hata kidogo.. soma Ukweli.



1. Kuna upotoshwaji uliyofanywa na gazeti moja likidai kuwa Naibu Meya amejiingiza katika biashara na kuchukua tenda ya kutengeneza Mabegi na Diari.


Jambo hili ni la Uongo na Upotoshaji, inayoonyesha nia ya kumchafua Mh Naibu Meya Prosper Msofe kwa nia ya kujenga taswira ya Chadema kutokuwa na viongozi makini. Jambo hili si la Kweli kabisa na Ukweli ni Kwamba tenda ya Mabegi na Diari ilitolewa kwa mujibu wa sheria na kupewa kwa kampuni ya Lewis Traders inayomilikiwa na Lewis.


Tunaomba wananchi na Wanachama wachadema waelewe kuwa hizo ni propaganda za watu wachache wasiokitakia Chama Chetu cha Chadema Mema na kumtakia mema Kiongozi wetu Naibu Meya Prosper Msofe. Naibu Meya ameonyesha kuwa Mchapakazi Hodari na Mbunifu kwa muda mfupi aliyopata fursa Hiyo.


Tuendelee kumuunga mkono Naibu Meya Mh. Proper Msofe kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumekiunga mkono chama Chetu Chadema, ambayo ndio Tumaini pekee la Watanzania. Kwa ushahidi zaidi, hizi hapa Stakabadhi za malipo ya vifaa hivyo na kampuni inayofanya kazi hiyo:




2. Kuna upotoshaji mkubwa uliofanywa na gazeti flani, likidai kuwa kuna mgogoro wa kisiasa katika Madiwani wa Chadema Arusha Mjini, Jambo hili si la kweli kabisa.


Ukweli ni kwamba katika moja ya vikao vya madiwani wa Chadema Arusha mjini, kuliibuliwa Hoja ya Kumchagua Mwenyekiti wa Madiwani mpya baada ya mjumbe huyo wa kikao kueleza kuwa anaona kuwa viatu hivyo vimepaya kwa aliyevivaa sasa. Kimsingi baadhi ya Madiwani wametathimini na kuona wanauhitaji wa kuwa na Mwenyekiti Mpya kutokana na mtazamo wao mpya wa kukiimarisha chama.


Hivyo baada ya kuibuka kwa hoja hiyo wajumbe walikubaliana kupanga siku mwafaka wa kufanya Uchaguzi huo, kabla ya hilo kufanyika baadhi ya madiwani walitumiwa barua kutoka ofisi ya Chadema wilaya ikiwataka madiwani hao kujieleza kardi barua zilivyowataka.


Hakuna mgogoro wala matusi yaliyoibuka kwenye kikao hicho , isipokuwa kumekuwa na  kutofautiana kwa hoja, 
1.Kumeonekana kuwa Madiwani wa Zamani kutamani kuhodhi nafasi ndani na nje ya chama, kwa katika upatikanaji wa Naibu Meya wa Chadema, inaonekana haikuwaridhisha walioikosa nafasi hiyo ilihali wao ni madiwani wazamani. Kumeibuka changamoto kuwa Madiwani wanaoamini kuwa Naibu Meya alitakiwa kutoka miongoni ma madiwani wa Zamani, Wengine wakiamini kuwa Uchaguzi uliyofanyika na kumpata Naibu Meya ni halali na kimsingi Ameonyesha  kufanya kazi hata zaidi ya Meya Mwenyewe. 

2. Kuna changamoto inayojitokeza kwenye nafasi Mwenyekiti wa Madiwani wa sasa inaonekana kupwaya na uendeshaji wake wa majukumu kuwa si wakuridhisha, ambayo ilipelekea Madiwani kutamani kutumia Demokrasia yao kumpata kufanya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema.
 

Tukitumia uzoefu wa Bunge Kiongozi wa Kambi ya Upinzani kuwa ndiye mwenyekiti wa Chama imejenga Heshima kubwa kwa Wabunge wa Chadema ndani na nje ya Bunge.


Hivyo nao madiwani hao walitamani kuona Kiongozi wa Madiwani anayeweza kuiletea Chadema heshima zaidi na kuweza kuwaongoza Madiwani hao kwa Democrasia ya kweli na ni kwa uchaguzi tu ndio hilo lingewezekana.


Kwa msingi huo kilichojitokeza ni Uitaji wa Demokrasia ya kweli katika Madiwani wa Chadema Arusha Mjini, katika kutekeleza chama kuwa ni cha Democrasia na Maendeleo. 
Pia kuondoa dhana kuwa mtu akichaguliwa nafasi Fulani akishinda kutekeleza majukumu yake kama ilivyoitajika hataondolewa. Ifahamike kuwa Chadema ndio Chama pekee kinachoweza kukemea viongozi ake na hata kuwawajibisha kwa kufuta Katiba na kanuni zilizoweka na Chama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad