MH. JOSHUA NASSARI AHAMISHIWA KCMC KWA MATIBABU ZAIDI YA MAJERAHA ALIYOPATA KWENYE MCHAKATO WA MADIWANI - MAKUYUNI ,ARUSHA. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Jun 2013

MH. JOSHUA NASSARI AHAMISHIWA KCMC KWA MATIBABU ZAIDI YA MAJERAHA ALIYOPATA KWENYE MCHAKATO WA MADIWANI - MAKUYUNI ,ARUSHA.



 Mbunge wa Arumeru Mashariki -Chadema Joshua Nassari akiwa wodini  hospitali ya selian Jijini Arusha
 Mbunge wa Arumeru Mashariki -Chadema Joshua Nassari muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya selian Jijini Arusha
--
 Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mhe. Joshua Nassari amehamishiwa katika hospitali ya KCMC-Moshi mkoani Kilimanjaro, kutokana na maumivu ya mgongo yanayomsumbua mara baada ya kupigwa katika kata ya makuyuni Mkoani Arusha wakati uchaguzi mdogo wa Madiwani ukiendelea.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari  amepigwa na kujeruhiwa vibaya , amepigwa na vijana wa kisomali, katika eneo la Zaburi kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli, Taarifa za awali zinasema baada ya Nassari kuondoka na gari  jingine, waliokuwa wanafuatana naye walienda kujibanza sehemu.

 Kiongozi wa Chadema aliyetambulika kwa jina la Teddy Ndossi na dereva wa Nassari. Dereva wa Nassari Guardian  Pallangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili, na kwa sasa wamempiga tena Katibu wa Chadema wa eneo hilo anayeitwa Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad