DR. GHARIB BILAL AAGANA NA MABALOZI WATEULE WA TANZANIA WANAOKWENDA KURIPOTI KWENYE VITUO VIPYA VYA KAZI. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Jun 2013

DR. GHARIB BILAL AAGANA NA MABALOZI WATEULE WA TANZANIA WANAOKWENDA KURIPOTI KWENYE VITUO VIPYA VYA KAZI.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva (kulia) ni Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad