BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE TAYARI KWA MTANANGE JUMAMOSI NDANI YA UWANJA WA JAMHURI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


12 Jun 2013

BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE TAYARI KWA MTANANGE JUMAMOSI NDANI YA UWANJA WA JAMHURI

 Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB  kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.Kwa mbaali namuona CEO wa Lukaza Blog.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
 Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.
Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Jamhuri Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili. Kwa hisani ya Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad