TANESCO YAIBUKA MSHINDI WA KERO KWA WATEJA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Nov 2012

TANESCO YAIBUKA MSHINDI WA KERO KWA WATEJA



TANESCO yaibuka mshindi katika mzunguko wa kwanza

Na Waaandishi wetu , hudumabongo@gmail.com

Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania (TANESCO)  limeibuka mshindi wa jumla wa kero kwa wateja wa huduma mbalimbali na  bidhaa hapa nchini kupitia mchakato unaoendelea kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook. Nafasi ya pili ilishikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na ya tatu kuchukuliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Katika mzunguko wa kwanza jumla ya makampuni 29 yaliingia katika kinyanganyiro na kufanikiwa kuchukua ushindi katika makundi mbalimbali .
Katika kundi la huduma za usafiri wa Anga , Shirika la Ndege la Precision ndio liliongoza kwa kero na huduma zisizo na uhakika huku kundi la huduma za maji likishikiliwa na Dawasco.
Kwa upande wa usafiri wa mabasi Kampuni ya Happy Nation iliongoza kwa malalamiko kutoka kwa wateja huku kundi la ving’amuzi vya Televisheni likiongozwa  na Star Times.
Kwa upande wa huduma za maegesho ya magari , eneo la Magogoni Ferry limelalamikiwa na wateja kwa huduma mbovu na kufanikiwa kushika nafasi za juu katika kundi hilo.
Kwa upande wa wateja wanaolipia huduma za Televisheni kituo cha TBC pekee ndicho kimelalamikiwa kwa kutokuwa na huduma za uhakika kwa watazamaji wake.
Katika kundi la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi , Kampuni ya Tigo ndiyo iliibuka  mshindi ikifuatiwa na Kampuni ya Vodacom.
Zoezi hili la kukusanya kero linafanywa na Wananchi  kupitia akaunti ya Twitter inayopatikana kupitia @hudumambayatz na facebook group iliyopewa jina la HUDUMA BONGO ambapo huduma na bidhaa zote zinazolipiwa na wateja mfano Burudani, Elimu, Hospitali, Hoteli, n.k zinazowakera wateja zitaingia katika kinyanganyiro hicho.
Washauri wa kibiashara wa Huduma Bongo wanatoa wito kwa viongozi wa juu wa Mashirika yote 29 yaliyotajwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wateja wao wanapata huduma bora kulingana na fedha wanazotoa ili kuweza kuleta maendeleo ya Taifa.
Zoezi hili linaendelea ambapo katika mzunguko wa kwanza jumla ya kero 119 ziliwasilishwa na wateja endapo msomaji una kero iliyoshindwa kupatiwa ufumbuzi na watoa huduma hawa unahitajika kuwa na akaunti inayotambulika ya Twitter au Facebook na kujiunga na Huduma Bongo kisha ueleze kero yako. Ukweli na Haki kuzingatiwa. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad