SHINDANO LA (DSTV EUTELST) LAPATA WASHINDI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Nov 2012

SHINDANO LA (DSTV EUTELST) LAPATA WASHINDI

Naibu Waziri wa Wizara ya  Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba  akitoa hotuba wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi  walioshinda shindano la kuandika Insha na Uchoraji Sayansi  (Dstv Eutelsat  Star  Awards)  washindi  wane kutoka shule za sekondari  walishinda baada  ya kufanyika mchuano mkali ambao ulishirikisha  zaidi ya wanafunzi 1000 katika shule mbalimbali za Afrika nzima,shindano hilo la tuzo liliandaliwa na MultiChoice kwa kushirikiana  na Eutelsat Communications.hafla hiyo ilifanyika kwenye Hotel ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice ,Bi.Barbara Kambogi(kulia)katibu Mhutasi  Multichoice(kushoto)Revina Bandihai.wakifuatilia kwa umakini hotuba iliyokuwa ikitolewa na  Naibu waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba  wakati  akitoa hotuba katika hafla  ya kuwapongeza washindi wa Dstv Eutelsat  Star  Awards.
Majaji wa shindano hilo wakiwa kwenye  picha ya pamoja  katika hafla hiyo.
Meneja masoko wa Multchoice  Furaha Samalu(kushoto)na Meneja masoko wa kampuni ya simu Zantel Awaichi Mawalla.wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu waziri wa Wizara ya Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba (watatu kushoto nyuma) Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel(wakwanza kulia nyuma)wakiwa kwenye picha ya pamoja na vingozi wengine,mbele kulia ni wanafunzi walioshinda tuzo ya Dstv Eutelsat Star.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Multchoice, Barbara Kambogi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo.PICHA NA PHILEMON SOLOMON

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad