Mahakama ya Rufaa Yatupilia Mbali Pingamizi Dhidi ya Rufaa Ya Godbless Lema Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


8 Nov 2012

Mahakama ya Rufaa Yatupilia Mbali Pingamizi Dhidi ya Rufaa Ya Godbless Lema Jijini Dar es Salaam


Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani, kupitia Wakili wao Alute Mughwai  ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe, limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.

Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za walio kata rufaa.

Mawakili wa Mh Godbless Lema wanahitajika kutimiza majalada ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matu

Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Tindu Lissu.

IMG-20121108-WA0007
IMG-20121108-WA0006

Baadhi ya wananchi, wapenzi wa Chadema wakimlaki Mh. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama.


IMG-20121108-WA0003Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mh. Godbless Lema.

IMG-20121108-WA0002Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam
IMG-20121108-WA0005Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu. 
Kwa hisani ya Arusha255.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad