KAMA UNA KERO YEYOTE, PITIA HAPA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Nov 2012

KAMA UNA KERO YEYOTE, PITIA HAPA


TAARIFA KWA UMMA

Uzinduzi wa Shindano la kusaka Mabingwa wa Kero kwa Wateja

Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter wamezindua rasmi shindano la kusaka kampuni inayotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.
Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, viongozi wa makampuni mbalimbali nchini na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara au watoa huduma mbalimbali nchini kutoa huduma bora kwa wananchi haswa ikizingatiwa wateja hawa hutumia fedha zao kulipia huduma na bidhaa hizo . Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.
Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa kulalamikiwa na wateja wao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni kampuni zipi zinashikilia usukani fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai ya Twitter au ya Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utakuwa umeifanya kampuni ulioitaja kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma Bongo inatoa wito kwa wakazi wa Arusha ambao kero zao zimeshindwa kutafutiwa ufumbuzi kushiriki kwa wingi katika shindao hilo ili kukomesha tabia hizi zinazorudisha maendeleo nyuma maendeleo ya Taifa.

Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo - hudumabongo@gmail.com


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad