DR. GHARIB BILAL KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KITAIFA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Nov 2012

DR. GHARIB BILAL KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KITAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kuhusu matumizi na makusudio ya mafunzo ya Kompyuta wakati alipotembelea katika chumba cha Kompyuta, baada ya kuzindua rasmi shule ya Msingi, Kiromo, leo Nov 27, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sam Elangalloor, wakati alipokuwa akitembelea katika Chumba cha Maktaba cha Shule ya Msingi Kiromo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kukagua maeneo ya Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo, shuleni hapo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliofanywa na kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakati akionyeshwa madawati yaliyotolewa na Kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mjumbe wa NEC Taifa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM, baada ya kuzindua rasmi Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Wilaya ya Bagamoyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mjumbe wa NEC Taifa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wanachama wa CCM, baada ya kuzindua rasmi Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Wilaya ya Bagamoyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Sheikh Mkuu wa Bagamoyo, Sheikh Abdallah Masoud Jembe, anayesumbuliwa na maradhi, wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Sheikh huyo, eneo la Ramiah mjini Bagamoyo, kwa ajili ya kumjulia hali. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Sheikh wa Bagamoyo, Sheikh Abdallah Masoud Jembe, wakati alipofika nyumbani kwa sheikh huyo eneo la Ramiah mjini Bagamoyo, leo Nov 27, 2012 kwa ajili ya kumjulia hali kutokana na maradhi yanayomsumbua sheikh huyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Gadiola Emanuel

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad